Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali: Tanzania ni salama kwa uwekezaji Afrika

Uchumi Kupanda Serikali: Tanzania ni salama kwa uwekezaji Afrika

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesihi wawekezaji na wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali kuja kuwekeza nchini kwani hali ya uwekezaji na mazingira ya ufanyaji biashara ni salama.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Wazalishaji wa Tanzania (TIMEXP), Naibu Waziri Kigahe amesema Serikali imehakikisha mazingira ya uwekezaji ni rafiki na hivyo waje kwa wingi kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Amesema hata mazingira ya ufanyaji biashara bado ni rafiki na hivyo kuwataka wafanyabiashara kuichagua Tanzania katika biashara zao.

Maonesho ya kimataifa ya wazalishaji wa viwanda Tanzania (TIMEXP) yanafanyika kwa siku tatu na yanashirikisha wazalishaji wa ndani na nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live