Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali, TBL Waingia Mkataba zao la zabibu

Fa5817c678856955bf23614337fb3fee Serikali, TBL Waingia Mkataba zao la zabibu

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amesema serikali imekubaliana na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwenye kilimo cha mkataba cha zao la zabibu ili kuwatafutia soko la uhakika wakulima wa zabibu mkoani Dodoma.

Bashe ameyasema hayo jana wakati wa kikao cha pamoja baina ya uongozi wa Wizara ya Kilimo na Menejimenti ya TBL juu ya namna ambavyo Kampuni hiyo itanunua mazao kwa wakulima katika utengenezaji wa bidhaa zake mbalimbali.

Katika majadiliano hayo, TBL wamekubaliana na serikali kuingia mikataba na wakulima wa zabibu wa mkoani Dodoma na kuwaelekeza viongozi wa TBL kushirikiana na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde kukamilisha mchakato huo.

Waziri Bashe amebainisha kuwa Wizara ya Kilimo inaamini kuwa wakulima wakiwa na makubaliano ya moja kwa moja na wakulima itawasaidia wakulima wa Tanzania na TBL itarahisha kazi katika kumfikia mkulima kwani kwa sasa ili TBL imfikie mkulima.

Kuhusu hitaji la kupata ardhi, Bashe amesema tayari serikali imeshawapa hekari 250 mkoani Dodoma.

Akitoa shukrani kwa Wizara ya Kilimo Mkurugenzi Mkaazi wa TBL Jose Moran amesema watafuata makubaliano waliyokubaliana na serikali kwani wamejidhatiti kuunga mkono juhudi za wakulima wa Tanzania na wataendelea kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Kilimo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live