Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana amefanya ziara katika mradi wa Liganga na Mchuchuma na kusema kuwa serikali inaendelea na makubaliano ya kimkataba na mwekezaji wa miradi hiyo ili iweze kuanza kufanya kazi hivi karibuni.
Waziri Chana ameongeza kuwa kuanza kwa miradi hiyo ni fursa ya kipekee kwa wakazi husika katika kuanzisha shughuli mbalimbali za kibiashara huku akiwasihi kudumisha amani na sheria za nchi kwani kutakuwa na muingiliano mkubwa wa watu.
Stanley Kolimba ni Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani Ludewa ameiomba serikali kuharakisha mchakato huo ili uweze kuanza kwani umekuwa ukizungumziwa kwa kipindi kirefu huku Meneja mradi wa Liganga na Mchuchuma kutoka Shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Witness Shuza akieleza mpango mkakati uliopo.