Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali: Magari chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

Magari 88 Serikali: Magari chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

Mon, 11 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema magari yaliyotengenezwa chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

Amesema; “Tanzania haitakiwi kuwa dampo kwa kuleta magari yaliyopitwa na wakati. Bunge letu limeshapitisha Sheria magari yote yanayoingizwa nchini yawe yametengenezwa baada ya mwaka 2010 kuja huku mbele. Huo ni wajibu wa TBS, lazima wajiridhishe na kuelimisha wanaoagiza magari,” amesema Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu ameitaka Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) kuimarisha utendaji kazi wake ikiwemo kuacha kuchelewesha ushushaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live