Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali: Kodi ya pango kukusanywa na TRA

Malamba4 1 Kodi ya pango kukusanywa na TRA

Tue, 20 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba amesimama Bungeni leo September 20, 2022 na kutoa kauli ya Serikali kuhusu tozo ambapo ameeleza marekebisho yatakayofanyika na kuanza kutumika kuanzia October 1, 2022

Waziri Mwigulu amesema “Serikali inafuta utaratibu wa kodi ya zuio inayotokana na pango kukusanywa na Mpangaji na badala yake jukumu hilo linarejeshwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa utaratibu utakao bainishwa kwenye kanuni”

“Napenda kusisitiza kuwa kodi ya zuio ya pango sio ya Mpangaji bali inapaswa kulipwa na Mpangishaji ambaye ndiye anapokea mapato kutokana na uwekezaji au biashara ya kupangisha”

“Utaratibu huo umekuwa ukitumika kwa muda mrefu kwenye nyumba za biashara na nyumba zinazopangishwa kwenye makampuni au mashirika yanayofunga ritani za kodi”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live