Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sera, sheria ni mikakati kuelekea uchumi wa viwanda

20870 KATIBU+PIC TanzaniaWeb

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk Edwin Mhede amesema sera, sheria na mikakati ni hatua moja ya kuelekea uchumi wa viwanda.

Amesema jambo kubwa ni kuimarisha mazingira ya nje na ndani katika kuimarisha viwanda.

Akizungumza leo usiku Oktoba 4, 2018 katika Jukwaa la Fikra la Mwananchi linalolenga kujadili fursa, changamoto na ufumbuzi kuelekea uchumi wa viwanda ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Dk Mhede amesema ili kuufikia uchumi wa viwanda  zipo sheria, sera na mikakati iliyowekwa.

Ametaja baadhi yake, Dk Mhende ipo ya masoko, kuendeleza viwanda vidogo na sera ya biashara.

Dk Mhede amesema licha ya sera hizo, Serikali iliunda mifumo ya udhibiti ikiwamo kuanzishwa kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Vipimo (WMA).

Ameeleza kuwa Serikali ipo kwenye mchakato wa kuboresha utekelezaji wa mpango wa kuondoa vikwazo vya biashara ambao tayari umeanza kuonyesha mafanikio.

"Katika kuimarisha mpango huo, tayari baadhi ya taasisi za Serikali zinazotoa huduma zinazofanana, zimeanza kusaini makubaliano," amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz