Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Selcom na NALA waingia makubaliano kuongeza nguvu kutuma fedha nje

SEM Selcom na NALA waingia makubaliano kuongeza nguvu kutuma fedha nje

Tue, 28 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Selcom na NALA wameingia makubaliano ya kushirikiana na kuongeza nguvu ya kutuma fedha kutoka nchi za nje (Uingereza na Marekani) moja kwa moja kwenda kwenye mitandao yote ya simu za mkononi na akaunti za kibenki nchini Tanzania.

Selcom ambao ni watoaji huduma wakubwa wa malipo nchini Tanzania, wametangaza ushirikiano huo wa kimkakati na NALA, kampuni ya kivumbuzi ya yenye makao yake makuu nchini Uingereza, utakaowezesha kuchochea miamala ya moja kwa moja kutoka nchi hizo mbili wakati wowote.

Ushirikiano na Selcom unasaidia kuiweka NALA katika mstari wa mbele katika kasi ya mapinduzi ya utumaji pesa ndani na nje ya nchi. Kasi hii ya mapinduzi inapewa nguvu kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Selcom katika ikolojia wa huduma za kifedha kama njia muhimu na uwezo wa NALA katika uvumbuzi bora wa bidhaa na huduma.

Kwa ushirikiano huu, watumiaji wa NALA nchini Uingereza na Marekani sasa wanaweza kuhamisha fedha kwenda benki kadhaa na kufanya miamala ya simu za mkononi nchini Tanzania kwa urahisi popote walipo. Hii pia itawapa watanzania waishio ughaibuni fursa ya kutuma mitaji nchini.

Mwaka 2021, Tanzania ilipokea dola milioni 570 kama fedha kutoka nje ya nchi, kutoka dola milioni 400 mwaka 2020. Mwaka 2022, Selcom inatarajia kufanya kazi kwa karibu na NALA, Serikali na mashirika mingine ili kukuza mapato zaidi kupitia uwekezaji katika sekta kama vile elimu, afya na kilimo. Wakati huohuo, NALA inaendelea kuendeleza dhamira yake ya kukuza fursa za kiuchumi kwa Afrika kwa kujenga masuluhisho nyeti ya kifedha.

Katika maelezo yake, Sameer Hirji, Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom,alisema, "tunafuraha kushirikiana na NALA, chapa iliyoanzishwa katika dhamira ya kuongeza fursa katika bara la Afrika na kwa wanadiaspora duniani kote. Kupitia uzoefu na uwezo wetu kama Selcom itakuwa nyongeza muhimu na ya kimkakati kudumisha huduma za kifedha nchini kushirikiana na huduma za kifedha za kijamii kutoka NALA’.

Aliendelea kusema, ‘ushirikiano wetu utawawezesha wateja wa NALA kutuma pesa kwa njia ya uwazi na ufanisi, hivyo kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya wateja wa NALA nchini Tanzania na kuunda njia mpya ya utumaji fedha kwa watu wanaoishi nje ya Afrika ili waweze kutuma pesa nyumbani na kwa msaada wa Benki Kuu na washirika kama vile NALA tunatarajia kuleta matokeo yanayoonekana."

Benjamin Fernandes, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa NALA aliongeza kuwa, "Ushirikiano na Selcom ni ishara ya nia yetu ya kuimarisha uwepo wa NALA katika masoko tuliyoyapa kipaumbele. Kama Mtanzania, inanifurahisha sana kuwekeza katika nchi yetu na ughaibuni.

Aliendelea, ‘Afrika ndilo bara ghali zaidi duniani kutuma pesa, na lengo la NALA ni kubadilisha dhana hiyo kwa kuunda masuluhisho ya kifedha ambayo Waafrika wanastahili. Na tunapozidi kupanua bidhaa zetu ili kuwafikia watu wengi zaidi, inakuwa muhimu zaidi kupata washirika muhimu ili kutimiza azma hii’.

Kupitia ushirikiano huu mpya inaendelea kuiweka Selcom kama chaguo sahihi kwa kampuni bunifu kama vile NALA kuzidi kukua kwasababu ya uwezo wa Selcom kujenga miundombinu ya malipo ya kifedha kimataifa amabayo pia inaunganisha taasisi za fedha kama vile benki na simu za mkononi kirahisi na kwa uaminifu.

Makampuni yote mawili yanaamini kuwa ushirikiano huu wa mwanzo ni kiashiria tosha kudumisha safari mapinduzi katika tasnia ya utumaji fedha nchini Tanzania na sambamba na kukuza upokeaji wa fedha kutoka nchi za nje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live