Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta ya uvuvi kurasimishwa

Samiaa Ikulu E Sekta ya uvuvi kurasimishwa

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa wanachukua hatua kurasimisha sekta ya uvuvi na kuwa ajira rasmi.

Rais Samia amesema hayo leo Januari 30,2024 jijini Mwanza baada ya kuhudhuria hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa wavuvi.

Amesema kwa muda mrefu sekta ya uvuvi ilikuwa kwenye ajira zisizo rasmi. Amefafanua kuwa baada ya hatua ya kurasimisha, kuwepo pia na rekodi za wavuvi na wote wanaoshughulika kwenye sekta hiyo pamoja na wachakataji wa mazao yanayohusu uvuvi .

Katika ziara yake ya kutembelea mialo na kukagua zana za uvuvi mkoani Mwanza aliyoifanya Oktoba 24, 2024; Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema ununuaji na utengenezaji zana za uvuvi unagharimu zaidi ya Sh25 bilioni, ikiwemo kujenga vizimba 615 vya ufugaji wa samaki na ununuzi wa boti, nyavu, vifaa vya usalama majini na vya kubaini samaki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live