Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta ya uchukuzi yachangia dola bilioni 2

Waziri Mbarawa: Serikali Kuendelea Kutoa Huduma Za Udhibiti Huduma Za Bandari Sekta ya uchukuzi yachangia dola bilioni 2

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Wizara ya Uchukuzi imeendelea kutoa mchango mkubwa wa ukuaji wa Uchumi kwa Taifa kwa kuwa ni sekta wezeshi katika kuchagiza ukuaji wa sekta nyingine za uzalishaji zikiwemo sekta za kilimo, madini, utalii, viwanda na biashara. Mathalan, katika mwaka 2022 Sekta ya Uchukuzi ilikua kwa asilimia 3.80 na kuchangia katika Pato la Taifa kwa asilimia 6.70. Aidha, Sekta hii ni ya tatu (3) kwa kuchangia fedha za kigeni kupitia mauzo ya huduma (Trade in Services).

“Wizara ya Uchukuzi imeendelea kutoa mchango mkubwa wa ukuaji wa Uchumi kwa Taifa kwa kuwa ni sekta wezeshi katika kuchagiza ukuaji wa sekta nyingine za uzalishaji zikiwemo sekta za kilimo, madini, utalii, viwanda na biashara. Mathalan, katika mwaka 2022 Sekta ya Uchukuzi ilikua kwa asilimia 3.80 na kuchangia katika Pato la Taifa kwa asilimia 6.70. Aidha, Sekta hii ni ya tatu (3) kwa kuchangia fedha za kigeni kupitia mauzo ya huduma (Trade in Services). Aidha, katika kipindi cha miaka mitatu, mchango wa sekta hii katika fedha za kigeni umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka Dola za Marekani bilioni 1.6 mwaka 2022 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 2.4 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 50 katika kipindi hicho”- Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live