Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta ya Posta kurekebishwa kuendana na soko

6738cb09f11812cf1341cee1c00d1c34 Sekta ya Posta kurekebishwa kuendana na soko

Sun, 25 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imesema itahakikisha inaendelea kufanya maboresho katika sekta ya posta ili iendane na mahitaji ya soko na matarajio ya wananchi.

Aidha, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iko mbioni kufufua upimaji wa huduma za posta kiteknolojia kwa kununua mtambo kutoka Umoja wa Posta Duniani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka wizara hiyo, Clarence Ichwekeleza alisema wizara inafanya mapitio ya sera inayoongoza sekta hiyo ili kujumuisha maendeleo ya teknolojia katika utoaji wa huduma za posta.

Alisema pia wanaendelea kutekeleza maazimio ya kimataifa yenye manufaa kwa nchi na maendeleo ya sekta kwa kushiriki kutoa michango.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Emmanuel Manase alisema mamlaka hiyo inatakiwa kupima utendaji wa shirika kama uko sambamba na viwango vya ubora vinavyotakiwa na taratibu za kimataifa.

“TCRA iko mbioni kufufua upimaji wa huduma za posta kiteknolojia kwa kununua mtambo wa Global Monitoring System (GMS) ambao utatusaidia kwa kiasi kikubwa kutoa takwimu sahihi za ubora wa huduma za usafirishaji wa posta," alisema Dk Manase.

Posta Masta Mkuu, Hussen Mwang'ombe alisema sekta ya posta inabadilika haraka kutokana na huduma zake kupitia kwenye mabadiliko makubwa yatokanayo na maendeleo ya teknolojia na kuwa wamejipanga vyema na mabadiliko hayo na kwamba wanatarajia kuzindua utoaji wa huduma kidijitali zinazojulikana kama Posta kiganjani.

Chanzo: www.habarileo.co.tz