Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta tano zitakazochochea viwanda SADC zabainishwa

Wed, 14 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC) imetaja sekta tano nyeti zitakazosaidia kuchochea utekelezaji wa shughuli za uanzishaji na ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara miongoni mwa nchi 16 wanachama wa jumuiya hiyo.

Katika kufanikisha Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Miundombinu katika mtangamano (RIDMP), utakaofikia ukomo wake 2027,  idara hiyo imesema uimarishaji wa sekta usafirishaji, nishati, Teknolojia ya habari na Mawasiliano (Tehama), vyanzo vya maji na hali ya hewa ndiyo msingi wa viwanda SADC.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu Agosti 12, 2019, Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, Mkurugenzi wa Huduma na Maendeleo ya Viwanda wa SADC, Mapolao Mokoena amesema usafirishaji wa bidhaa miongoni mwa nchi wanachama hautafanikiwa bila kukamilika kwa barabara imara zinazounganisha jumuiya hiyo.

Napolao amesema kila nchi inalazimika kuimarisha miundombinu hiyo ili kuharakisha upatikanaji wa huduma hizo, kwa lengo la kupunguza umaskini na kufikia malengo la Endelevu ya Milenia(SDG).

“Miundombinu ndiyo moyo wa viwanda na biashara, huwezi kusafirisha bidhaa bila kuwa na miundombinu imara,” amesema.

“Malengo ya sekta ya usafirishaji ni kufanikisha ubora, uharaka na uwezo wa miundombinu kutoa huduma katika barabara, njia za reli, huduma za anga na Majini, huduma za bandari, eneo muhimu ni mifumo ya logistics, kuoanisha sera, uwezeshaji,” amesema.

Pia Soma

 

“Maendeleo ya shughuli za ujenzi wa barabara pia yanalenga kufanikisha ukuaji wa soko huru la kibiashara ndani ya mtangamano.”

Amesema sekta ya nishati ndiyo inasaidia zaidi kukuza uzalishaji na kupunguza gharama za manunuzi ya bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa kwa mtumiaji wa mwisho.

“Hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme hairidhishi katika jumuiya hiyo, Tanzania imeonyesha dhamira ya kukabiliana na changamoto hiyo kupitia mradi wake wa umeme (Mto Rufiji), kwa hiyo kila nchi inalazimika kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme ili kulisha nchi zenye mahitaji ndani ya jumuiya,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz