Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta binafsi yaruhusiwa kuingiza matrekta madogo

5221184e226944049da28d2e868a8101 Sekta binafsi yaruhusiwa kuingiza matrekta madogo

Wed, 10 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imeiruhusu sekta binafsi kuingiza nchini matrekta madogo aina ya power tiller ili kurahisisha ukuaji wa sekta ya kilimo nchini.

Hatua hiyo itakuwa na manufaa makubwa kutokana na wananchi wengi kujikita katika kilimo cha kutumia trekta na kuondokana na kilimo cha mazoea.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Utafiti wa Teknolojia ya Kilimo katika Bodi ya Maendeleo ya Rasilimali za Wanyama na Kilimo Rwanda (RAB), Dk Charles Bucagu alisema matrekta hayo madogo yatasaidia kukuza kilimo na sekta binafsi imepewa nafasi kubwa ya kuyaingiza nchini.

Takwimu zinaonesha zaidi ya asilimi 60 ya wakulima wadogo nchini wana eneo la kilimo chini ya nusu heka na kati yao wapo maeneo ya miinuko hivyo wanahitaji teknolojia wezeshi kama matumizi ya Power Tiller.

Bucagu alisema kuna baadhi ya wawekezaji vijana waliosoma kilimo Israel na Rwanda ambao hivi karibuni walionesha nia ya kuingiza nchini Power Tiller.

Ofisa Biashara Mkuu wa kampuni ya Yalla Yalla Group, Odile Mugisha kampuni inayomilikiwa na mfanyabiashara kijana wa mazao ya kilimo alisema Power Tiller moja gharama yake ni faranga milioni 2, lakini wakati baadhi ya wakulima wana uwezo wa kununua na wapo wanaoomba ruzuku ili kununua matrekta hayo.

“Wakati msimu wa kilimo ukikaribia, mahitaji kutoka kwa wakulima ni makubwa wakati Power Tiller ni chache,” alisena na kuongeza kuwa wakulima hulipa faranga 150,000 kulima heka moja ya ardhi, hivyo kutokana na mahitaji makubwa wamepanga kuingiza nchini zaidi ya Power Tiller 15 na kuwa na matawi nchi nzima.

Rwanda imepanga kuongeza eneo la kilimo kwa asilimia 27 kutoka za sasa asilimia 50 ifikapo 2024, kilimo cha umwagiliaji kikitarajiwa kuongezeka kutoka hekta 63,742 mpaka hekta 102,284 kufikia mwaka huo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz