Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta binafsi, wanaowajibika nayo waumiza vichwa safari endelevu

BINAFSI Sekta binafsi, wanaowajibika nayo waumiza vichwa safari endelevu

Fri, 10 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

• Kipato Kati; teknolojia kijani; jinsia

TANGU zamani sekta binafsi imekuwa na mchango muhimu katika kutokomeza umaskini na kuleta maendeleo ya kiuchumi.

Katika nchi zinazoendelea, sekta binafsi inatajwa kutoa nafasi za ajira tisa, kati ya 10 katika nchi zinazoendelea.

Ni sekta yenye majukumu muhimu ya kutekeleza katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kutatua matatizo ya dunia, ikileta ufanisi ulioboreshwa, matumizi ya teknolojia na uvumbuzi.

Katika semina iliyofanyika kwa njia ya mtandao yenye jina la ‘Ustahimilivu wa Sekta Binafsi’ ikilenga kuangalia jinsi uongozi wa pamoja unavyoweza kugeuza upotevu wa asili iliyofanyika jijini Dar es salaam.

Washiriki walikubaliana kila kampuni kwa kujitegemea, ikamate ajenda ya mazingira iliyoambatanishwa katika mpango wake wa uwekezaji jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Hisham Hendi, anasema kampuni hiyo ina falsafa na mchango katika kufikiwa maendeleo endelevu.

Anasema, uwajibikaji wa kampuni kupitia utendaji endelevu ni kipengele muhimu kwao na wametoa mwongozo kwa kila nyanja ya uwekezaji, utanuzi, ukuaji na utoaji wa huduma.

“Mkakati wetu wa kipindi cha kati unaendana vyema na Mipango ya Maendeleo ya Kitaifa ya Mwaka 2016/2021 na malengo ya maendeleo endelevu ambayo yameanzishwa, kuhamasisha Tanzania kutambua mpango wake wa kuwa na jamii ya kipato cha kati kufikia 2025,” anasema.

“Kazi yetu inaharakisha ujumuishwaji wa kifedha na kufanya kazi na makundi mbalimbali ya kijamii, makundi ya wanawake na vijana vile vile kusaidia kufikiwa SDG5 (usawa wa kijinsia),” anafafanua Hisham.

Naibu Mwakilishi mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Sergio Valdini, anahamasisha uimarishaji ushirikiano na sekta binafsi katika kufadhili na kuwezesha teknolojia ya kijani katika utendaji.

Balozi wa Norway nchini, Elizabeth Jacobsen, anasisitizia haja ya kuwapo juhudi zilizokubaliwa zinazohusu watendaji mbalimbali kuimarisha utendaji wa kibiashara katika uwajibikaji.

“Tunapaswa kuhamasisha jamii yenye uwazi na wadau mbalimbali kutekeleza majukumu yao katika majadiliano, kuhusu mazingira kwa lengo la kuchukua mawazo bora zaidi, kuhusu teknolojia ya kijani na ubunifu,” anasema Elizabeth.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bia Tanzania, Philip Redman, anasema dhana ya ‘uendelevu’ ni ya msingi kwenye biashara na sio kitu cha ziada, katika uhakikishaji kwamba mikakati uendelevu inasimikwa kama sehemu ya falsafa ya biashara.

Mchangiaji, Simon Shayo, Makamu Rais wa kampuni ya AngloGold Ashanti, anapongeza majadiliano hayo ya wazi ya wadau na ushirikiano uliopo kati ya mashirika ya kitaalamu kusaidia jitihada za serikali kuhakikisha ukuaji imara wa uchumi na kijamii, hatimaye kuchangia kufikiwa malengo yote 17 endelevu.

Sekta binafsi inaendelea kuwa na jukumu muhimu katika kufadhili na kuwezesha jitihada nyingi za uendelevu za kiserikali, jambo linalotajwa kuleta mabadiliko chanya katika jamii, ikiwamo manufaa ya kijamii, kiuchumi na kimazingira.

Ni semina iliyowaleta pamoja, viongozi kutoka taasisi mbalimbali za kibiashara na washirika wa maendeleo katika kuimarisha jitihada za pamoja.

Vilevile inatajwa kuwa mfano hao na mafunzo bora kuhusu jinsi ya kutumia mifumo yake katika kufikia malengo ya kibiashara na kuboresha maadili, utendaji salama kwa mazingira na kufadhili jitihada za kijani kuelekea kufikia malengo ya usawa wa kijinsia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live