Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta binafsi mwarobaini ajira kwa vijana

Ajira Mpyaaaaa Sekta binafsi mwarobaini ajira kwa vijana

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg. Rehema Sombi Omary (MNEC) amesema kuwa azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona Vijana wa kitanzania wanaenda kutengeneza Ukwasi na kuona kila kijana anajenga kesho iliyo bora.

Sombi ameeleza hayo alipoongoza wajumbe wa kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa kufanya ziara Kwenye Kiwanda cha ukataji wa tofali kutoka katika Miamba inayotokana na Volkano iliyokufa kwa kutengeneza Matofali (Rock Blocks, Paving stone, Cobble stone, Cabbly stone, hozorana).

"Pamoja na kile nilichokiona hapa Rombo kwa kiwanda hiki kilichoajiri vijana zaidi ya 200. nitoe pongezi kwa kijana mwenzetu Fabian Oisso kwa kuvaa ujasiri na Kuwekeza katika kiwanda hiki na niwaahidi Ushirikiano, Kuwasemea na kuwafungulia njia kwa Mikoa mingine kwa kuwatangazia bidhaa zenu." Amesema @rehema_sombi

Kufuatia changamoto zilizotajwa na Uongozi wa kiwanda hicho ikiwemo Miundombinu ya Barabara, Maji, Afya na Umeme Mkuu wa Wilaya ya Rombo ameahidi kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo Kwa kuanza kusogeza huduma ya awali (First Aid) Kwa watumishi wa kiwanda hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live