Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta binafsi ina mchango wa maendeleo

Serikali Imefanikiwa Kuwa Karibu Na Wananchi   Dk Mwinyi Sekta binafsi ina mchango wa maendeleo

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Sekta binafsi ina mchango wa kizalendo wa maendeleo wa kuhakikisha Tanzania inazidi kupiga hatua na kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi .

Dkt Mwinyi amesema wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Julai 2024.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Maazimio ya mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara yatakuwa ni dira kutatua changamoto zinazokabili shughuli za biashara nchini na kuwa mwongozo kwa Serikali, watendaji na wafanyabiashara katika kufungua ukurasa mpya wa mageuzi ya kidijiti .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live