Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta binafsi Tanzania, Uganda zajadili fursa bomba la mafuta

Bomba La Mafuta TANGA Wajadili fursa za bomba la mafuta

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: ippmedia.com

Sekta binafsi za Tanzania na Uganda zimeandaa kongamano litakalo kutanisha wafanyabiashara wa nchizo zote mbili ili kujadili na kutoa fursa za biashara kupitia mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Chongoleani Tanga.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Francis Nanai, akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema kongamano hilo litakalofanyika mkoani Dar es Salaam, litahusisha zaidi ya watu 2,000 kati yao kushiriki kwa njia ya mtandao.

Alisema lengo la kongamano ni kuwandaa Watanzania na Waganda, waliojiajiri kwenye sekta binafsi kujiandaa kuendesha miradi itakayohusiana na mradi huo ikiwamo, kampuni za uondoshaji na usafirishaji mizigo kutoka bandarini, zinazotoa huduma za hoteli na mfumo wa teknolojia wa kisasa.

“Mradi huu wa bomba lenye urefu wa kilomita 1,443 utakuwa na thamani ya uwekezaji dola za kimarekani bilioni 20, tunatarajia miradi ndani yake kwa wakazi wetu. Mkutano huu utafanyika Novemba 25, mwaka huu ni ushirikiano wa serikali mbili, Wizara ya Nishati na Wizara ya Mambo ya Nje Uganda kupitia ubalozi wake nchini,” alisema Nanai.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Uganda (PSFU), Dk. Elly Karuhanga, alisema ushirikiano wa sekta binafsi kwa nchi mbili utawanufaisha wakazi wake hususan kweye miradi itokanayo na maliasili.

“Kwenye mkutano huu tutapanga namna maliasili za nchi zetu zinavyoweza kutunufaisha hasa kupitia gesi na mafuta. Sekta binafsi zinatakiwa kufanya kazi yake zaidi, tayari serikali imeshafanya kwa nafasi yake, sekta binafsi tusiiangushe serikali,” alisema Dk. Karuhanga.

Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Godfrey Chibulunje, alisema tayari wazawa 1,011 wenye kampuni za kutoa huduma mbalimbali kwenye mradi wamejisajili ili kutoa huduma.

“Wiki mbili zilizopita walikuwa wamejisajili wenye kampuni takribani 700 hadi leo (jana) waliokwisha sajiliwa ni zaidi ya 1,000 utaona namna gani wazawa wanavyochangamkia fursa,” alisema Chibulunje.

Balozi wa Uganda nchini Tanzania Richard Kabonero, alitoa wito kwa sekta binafsi kwa nchi mbili, kushirikiana ili kubadilishana uzoefu kufungua milango ya kiuchumi.

Chanzo: ippmedia.com