Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saruji nyeupe kuitangaza Tanzania

White Cement A Strong Bond For The Future Saruji nyeupe kuitangaza Tanzania

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imezitaka halmashauri nchini kuendelea kuboresha miundombinu sanjari na kutenga maeneo rafiki kwa uwekezaji na wawekezaji ili kuifikia azma ya serikali kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema hayo wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani wakati akizindua kiwanda cha Fortune ambacho ni chakwanza kwa ukanda wa Nchi za Kusini Mwa Jangwa la Sahara, kinachozalisha saruji nyeupe kwa ajili ya ujenzi chenye uwezo wa kuzalisha tani 200 Kwa siku.

"Kuwekeza nchini Tanzania ni sehemu salama na yenye mazingira yaliyoboreshwa ambayo kila mwekezani ataweza kunufaika na wananchi nao kunufaika," amesema Kigahe na kuongeza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya kupunguzwa umaskini na kukuza uchumi wa nchi.

Amesema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hususani kupitia sekta ya viwanda Ili viweze kuchangia katika kuongeza fursa mbalimbali nchini, ikiwemo ajira, fedha za kigeni ili kuchangia kukuza uchumi wa nchi.

Amesema serikali itashirikiana kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda hicho zinavuka mipaka ya nchi na kufika hata katika soko huru la Afrika.

“Kiwanda hicho mbali ya kuongeza thamani ya uzalishaji lakini pia ni sehemu ya kuitangaza Tanzania,” amesisitiza Kigahe. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live