Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sarafu ya karne ya 8 Tanzania yapatikana Austaria

Karne Sarafu Kupatikana Sarafu ya karne ya 8 Tanzania yapatikana Austaria

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watafiti wa Australia wanashangazwa na fumbo linalohusishwa na Afrika ya kale. Sarafu zilizoundwa kwenye pwani ya Tanzania ya sasa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita zimegunduliwa kwenye visiwa visivyo na wakazi wengi kaskazini mwa Australia.

Upatikanaji wa sarafi hizo umeibua swali hili kwamba je, Waafrika waligundua eneo kubwa la Oceania muda mrefu kabla ya Wazungu wa Ulaya au la?

Sarafu zinazoaminika kutengenezwa karibu miaka 1,000 iliyopita katika Tanzania ya sasa zimegunduliwa nchini Australia, kulingana na jarida la African Australian.

Wataalamu wanasema sarafu tano za kale zilizogunduliwa katika Visiwa vya Wessel vilivyo mbali katika Wilaya ya Kaskazini mwa Australia ni za kipindi cha kati ya karne ya 8 na 15 Miladia. Sarafu hizo zimetengenezwa kwa shaba, fedha na dhahabu, na zilitengenezwa Kilwa, jiji lililo kwenye ufuo wa Tanzania ya leo.

Wataalamu wanasema yamkini sarafu hizo zilitumika kama sarafu ya biashara kati ya eneo la Oceania na Kilwa Kisiwani, ufalme wa kale uliokuwa na nguvu na ulikuwa maarufu kwa biashara ya dhahabu, pembe za ndovu, na bidhaa nyingine kutoka ndani ya Afrika na kuvuka Bahari ya Hindi hadi maeneo mengine duniani.

Kwa hiyo inawezekana wakaazi wa mwambao wa Afrika Mashariki katika zama za kale waliigundua Australia muda mrefu kabla ya Wazungu. Watafiti sasa wanajadili kadhia hiyo huku wengi wakiamini kuwa wafanyabiashara wa kale wa Afrika Mashariki wanaweza kuwa walitembelea Oceania mara kwa mara.

Njia za biashara zilianzia ndani kabisa ya Afrika hadi Bahari ya Hindi, ambapo wafanyabiashara waliondoka na kuelekea maeneo mengine ya ng'ambo.

Watafiti wa Australia wanakubali, hata hivyo, kwamba maelezo kamili ya uwepo wa sarafu hizo bado hayajaweza kubainika vizuri, na utafiti zaidi unahitajika ili kuthibitisha asili ya sarafu hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live