Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sarafu ya Euro yashuka na kufikia thamani sawa na dola

Euro Usd Sarafu ya Euro yashuka na kufikia thamani sawa na dola

Wed, 13 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara ya kwanza, sarafu ya Euro imeshuka na kufikia ukingo wa usawa na thamani ya dola ya Marekani.

Hii itatokea ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20 huku hofu ikizidi kutanda baada ya Urusi kutangaza kukata usambazaji wa gesi kwenye nchi za Bara la Ulaya.

Bomba kubwa la gesi, Nord Stream 1 linalosafirisha gesi hiyo kutoka Urusi kwenda Ujerumani limeanza kufanyiwa matengenezo makubwa ya mwaka kuanzia juzi Jumatatu ambapo usafirishaji umesitishwa kwa muda wa siku 10.

Urusi imepunguza usambazaji wa gesi kwa baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya ikiwemo kupunguza kwa 60% huku viongozi wa Ulaya wakisema huenda gesi hiyo imesitishwa kutokana na vita vya Ukraine.

Reuters wameripoti kwamba Euro ilifikia dola $1.0051 jana Jumanne ikiwa ni chini ya takriban 12% tangu kuanza kwa mwaka huku hofu ya mdororo wa uchumi ikiongezeka kutokana na kuchochewa na mfumuko wa bei na kutokuwa na uhakika wa usambazaji wa nishati kunakosababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Umoja wa Ulaya ambao ulipokea takriban 40% ya gesi yake kupitia mabomba ya Urusi kabla ya vita, unajaribu kupunguza utegemezi wake kwa mafuta na gesi ya Urusi wakati huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live