Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sarafu moja EAC bado sana...

Eac Sudan.jpeg Sarafu moja EAC bado sana...

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NCHI Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zipo katika mchakato wa kuunganisha sera na kuwa na taasisi zinazohitajika kwa ajili ya kuwa na sarafu moja kama ilivyoainishwa kwenye Itifaki ya Umoja wa Fedha wa EAC.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopo kwenye mtandao wa WhatsApp wa EAC Integration, Itifaki ya Umoja wa Fedha wa EAC iliyosainiwa Novemba 30, 2013 inalenga kuunganisha sarafu za nchi washirika ili kuwa moja.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa endapo sarafu za nchi zote wanachama katika kipindi cha miaka 10 iliyopita zingeunganishwa ili kuwa na moja, jumuiya hiyo ingefanikiwa kuwa na sarafu moja mwaka huu wa 2024. Ili kuwa na sarafu moja, imeelezwa kuwa nchi wanachama zinapaswa kuunganisha sera zao za fedha pamoja na mifumo ya kifedha na malipo.

Aidha, taarifa hiyo ilisema kuwapo kwa sarafu moja kutawezesha kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Afrika Mashariki ambayo itatanguliwa na uundwaji wa Taasisi ya Fedha ya Afrika Mashariki (EAMI). Ilieleza kuwa ucheleweshaji wa utekelezaji wa itifaki hiyo unaathiri manufaa yaliyotarajiwa ikiwamo kufanyika kwa urahisi miamala ya kifedha na kuondoa changamoto ya ubadilishaji fedha mipakani.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa majadiliano kuhusu suala hilo yatakuwa kwenye ajenda ya Mkutano wa 27 wa Pamoja wa Kamati ya Masuala ya Fedha ya EAC unaofanyika Juba, Sudan Kusini kuanzia

Chanzo: www.tanzaniaweb.live