Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samsung yazidi kujiimarisha Tanzania

Samy Wadau wa Mawasiliano wakitazamaa vifaa vya Samsung

Thu, 17 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Samsung Afrika Mashariki imekutana na kuzungumza na wadau wake wa kibiashara ili kuimarisha uhusiano na kujadili matumizi bora ya bidhaa zake kwa wananchi wa Tanzania.

Kampuni ya Samsung inaamini kuwa maendeleo ya kiteknolojia ndiyo kichocheo kikuu cha biashara ya bidhaa zake ulimwenguni.

Mazungumzo hayo ambayo ni sehemu ya kuimarisha uhusiano na wateja wake, yamefanyika katika hoteli ya Hayatt Jijini Dar es Salaam yakiwakutanisha wafanyabiashara na wasambazaji wa bidhaa zake kutoka pande zote Tanzania.

Mkutano huo umeandaliwa na Mkurugenzi Mkuu mpya wa kampuni ya Samsung Afrika Mashariki, Tae Sun Lee na kuwaleta pamoja wadau wakuu wa bidhaa za Samsung wakiwemo wasambazaji na wafanyabishara ili kuhakikisha matumizi bora yanatolewa kwa watumiaji wa bidhaa za Samsung.

Mkurugenzi Mkuu wa Samsung, Lee amesema kuwa kampuni ya Samsung itaendelea kuimarisha uhusiano na washirika wake wakiwemo wasambazaji wote wa Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki.

Lee amesema kuwa Samsung itahakikisha bidhaa zote zinazotengenezwa na kampuni hiyo zinaendelea kuwa zenye ubora wa hali ya juu ili kumpa furaha na faraja mtumiaji wake.

"Kama Samsung tunasisitiza kuwa tutaendelea kuwa na sauti moja pale tunapoweka mikakati yetu ili tuweze kwenda mbele. Mienendo yetu ya soko inaendelea kubadilika na pia tunaona haja ya kurekebisha katika maeneo mbali mbali ili kukidhi mahitaji ya wadau,” amesema Lee.

Aidha, amesema mkakati wa kampuni hiyo ni kuona bidhaa zake za kielektroniki zinaendelea kukubalika katika soko la Afrika.

Katika mkutano huo, bidhaa mbalimbali za kampuni ya Samsung za mwaka 2022 zimeonyeshwa zikiwemo simu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live