Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samsung na Tigo waungana kuzindua toleo jipya la simu

98989 Pic+sumsung Samsung na Tigo waungana kuzindua toleo jipya la simu

Fri, 13 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na Samsung Electronics leo wamezindua simu  aina ya Samsung S20 nchini Tanzania. Simu hizo tatu ni Galaxy S20, Galaxy S20+ na Galaxy S20 Ultra.

Taarifa iliyotilewa na makampuni hayo inasema ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati wa kuongea matumizi ya mtandao wa 4G na kuchangia ukuaji wa teknolojia ya kidigitali nchini.

Meneja wa bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Muyonga akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo alisema kuwa ni jambo la kujivunia kuchaguliwa na Samsung kuwa wa kwanza kuzihifadhi na kuuza simu za Samsung S20 kwenye soko la Tanzania.

“Hii inaonesha imani yao kwetu juu ya chaneli kubwa za usambazaji tulizonazo na pia kupitia timu yetu ya huduma kwa wateja inayotoa huduma zenye ubora wa hali ya juu,”alisema Muyonga.

 Aliongeza: Lengo letu ni kuchochea mageuzi ya kidigitali katika maisha ya watu hapa nchini na ndio maana tumeungana na Samsung ili kuongeza idadi ya umiliki wa simu janja pamoja na matumizi ya data ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanaifikiwa na teknolojia hii.

Muyonga aliongeza  kuwa Tigo inalenga kuongeza ueneaji wa simu janja nchini huku wakihakikisha wateja wao wanafurahia huduma za kidigitali kupitia mtandao mkubwa wa 4G hapa nchini.

Pia Soma

Advertisement
“Na ndio maana tunatoa 78 Gb za intaneti kwa mwaka mzima kwa wateja wote watakaonununa Samsung S20,” alisema .

Akizungumza wakati wa  uzindizu huo, Meneja wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohamed alisema Samsung imezindua simu ya Samsung Galaxy S20 toleo jipya ulimwenguni ambayo itabadilisha namna ambavyo watu wanavyoishi na kuufurahia ulimwengu.

Galaxy S20 ina camera ambayo ina uwezo wa kipekee wa kupiga picha huku ikiwa na sifa mbalimbali ambazo zitamfanya mtumiaji kufurahia kuitumia ikiwamo muziki,video zenye ubora pamoja na michezo (games) mbalimbali.

“Tukiwa tunaingia kwenye muongo mwingine, kuna mabadiliko makubwa kwenye sekta ya mawasiliano na namna watu wanavyo ujua na kuufurahia ulimwengu.Samsung inahakikisha inatoa teknolojia na vifaa vya kisasa zaidi ili kuendana na mabadiliko hayo.Kwa kutumia camera yenye mfumo wa AI unaweza kupata kila tukio na kuungana na uwapendao bila mipaka,” alisema Mohamed.

Chanzo: mwananchi.co.tz