Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia atoa milioni 100/- za paa Machinga Complex

6008ed27589f552807737c7cb2e071d5.jpeg Samia atoa milioni 100/- za paa Machinga Complex

Thu, 22 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa Sh milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa paa la kisasa la kuzuia jua na mvua ili wafanyabiashara wa Kariakoo waliohamia katika Soko la Machinga Complex wafanye kazi kwenye mazingira mazuri.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewaeleza waandishi wa habari kuwa ameshapokea fedha hizo na ujenzi utaanza mara moja.

Juzi Makalla aliwatembelea wafanyabishara hao na kubaini changamoto hiyo na alipoulizwa na Rais Samia kiasi cha fedha kilichohitaji awali ilimweleza Sh milioni 62.

“Baada ya jana kuwatembelea na kuwasikiliza, Rais Samia aliona changamoto hiyo na aliniponiuliza cha fedha kinachohitajika nilimwambia ni milioni 62 za ujenzi wa paa la turubai lakini kwa kutambua umuhimu wa wafanyabiashara Rais Samia alitoa milioni 100 ili lijengwe paa la kudumu kwa bati la kisasa,” alisema Makalla.

Aliwataka Suma JKT ambao ndio wajenzi wa paa hilo waanze ujenzi mara moja ili wafanyabishara wafanye kazi bila kero.

“Kuhusu suala la meza tayari mkandarasi ameshapatikana na atajenga meza za kisasa za kuhamishika kuendana na hadhi ya soko,” alisema mkuu wa mkoa.

Alielekeza viongozi wa Jiji la Ilala waboreshe miundombinu ya taka, mifumo ya maji safi, mifumo ya umeme na wafunge vifaa vya kuzima moto.

Baadhi ya wafanyabiashara waliokumbwa na maafa ya kuungua Soko Kuu la Kariakoo wamefahamia sokoni hapo na katika soko la Kisutu.

Ofisa Masoko wa Jiji la Dar es Salaam, Victor Rugemalila alisema hadi jana zaidi ya wafanyabishara 2,054 walihamia katika masoko hayo wakiwemo 1,800 waliohamia Machinga Complex wakiwemo wafanyabishara wadogo (Machinga) 570 na 298 wapo soko la Kisutu.

Kwa upande wa soko la Kisutu, Makalla alielekeza kuwa waliopewa maeneo ya kujenga fremu waruhusiwe kuzijenga na wasizungushwe na gharama ziwekwe wazi.

Pia aliielekeza Halmashauri ya Jiji la Ilala kuwaondoa wafanyabiashara wanaoendesha biashara kwenye hifadhi za barabara na kuwatafutia vizimba ndani ya masoko hayo.

Akizungumza na Habari- LEO jana, Makamu Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo, Steve Lusinde alisema mchakato wa uhamiaji umekamilika kwa asilimia 85 na kwamba wamachinga 636 wanatakiwa kuhamia huku waliobaki wakiwa ni 66.

“Utaratibu wetu ni kwamba tunahamisha wamachinga 636 waliokuwa katika eneo hili la kariakoo na tunatarajia kumaliza wote wiki hii hadi ijumaa matarajio yetu yatakuwa yamekamilika,” alisema Lusinde.

Meneja wa Soko la Machinga Complex aliyejitambulisha kwa jina la Stella, alisema bado wanaendelea kupokea wafanyabishara katika soko hilo.

“Bado tunaendelea kupokea hadi sasa tuliowapokea wengi ni wa juu na maeneo ya nje bado wa ndani na tumeanza na wale wenye mazao ya kuoza wale ambao hawana vitu vya kuoza wanasubiri kwanza,” alisema Stella.

Chanzo: www.habarileo.co.tz