Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia ataka ukaguzi fedha za wananchi

Uamuzi Wa Rais Samia Wawakosha Wakazi Wa Nanyamba.jpeg Samia ataka ukaguzi fedha za wananchi

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kukaguliwa kwa fedha za wananchi zinazochangishwa mkoani Mtwara.

Ametoa agizo hilo akihutubia kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya Bomani Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi katika mkoa huo.

Sambamba na hilo Rais Samia amesema sio vibaya kwa wananchi kuchangishwa fedha hizo lakini mifuko inayohifadhi fedha hizo ijulikane, ikagukiwe na taarifa sahihi ya mifuko hiyo itolewe kwa kuwa ni fedha kutoka kwa wananchi

Aidha, amewataka viongozi wa ngazi zote kuacha kukaa ofisini na kushuka chini kusikiliza na kutatua kero za wananchi huku akionesha kusikitishwa kwa kuona kero za wananchi wa vijijini zinapelekwa Ikulu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live