Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia ataka mikopo halmshauri kutolewa benki

Fedhaa 0 Samia ataka mikopo halmshauri kutolewa benki

Thu, 30 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akipokea ripoti ya CAG na TAKUKURU Ikulu Dar es salaam leo amesema CAG amebaini kutokurejeshwa kwa Tsh. Bilioni 88 za waliokopa fedha 10% zinazotolewa na Halmashauri ambapo ameshauri fedha hizo zipelekwe Benki na Watu wakopeshwe na Benki hizo ili iwe rahisi kurejesha.

“Pesa za Halmashauri 10% tunaambiwa Bil 88 imekwenda haijakusanywa na haikusanyika, na hii ni kwasababu CAG amesema vikundi vinavyopewa ni hewa, uadilifu kwa Madiwani hakuna, pili hata vikundi vilivyopo vinajua tumepewa na Madiwani wetu, ni political funds ya Madiwani kwahiyo hawaoni umuhimu wa kurejesha

“Huku nako kunataka marekebisho, njia tunayotumia haitofanya kazi siku zote, njia nzuri ni kuingiza kwenye mfumo wa kibenki, hii fedha ikusanywe kila Halmashauri ipigiwe hesabu yake kwa mwaka huo 10% ni kiasi kadhaa ipelekwe kwenye Benki tutakayokubaliana baada ya kubadili mfumo”

“Ikakae Benki, Vijana, Wanawake wenye ulemavu wakachukue fedha Benki, kwasababu Benki utake utarudisha usipotaka utarudisha, hukufanya mradi utakwenda kuuza mbuzi wako au bangili lakini utarudisha Benki, tutaondoa pia ukiritimba wa Madiwani kufanya wanavyotaka, hii fedha bajeti ya mwakani iundiwe mfumo mpya”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live