Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia ataka kasi usimamizi wa miradi

Samia 08 04 At 14.jpeg Samia ataka kasi usimamizi wa miradi

Wed, 7 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Nishati kuongeza nguvu katika kusimamia miradi yote ya nishati ili ikamilike kwa wakati na hivyo kuwawezesha wananchi kupata nishati ya uhakika.

Rais Samia ametoa agizo hilo Agosti 06, 2024 wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

"Nimejionea mwenyewe wakati naenda Kilosa tofauti iliyokuwa ikionekana maeneo ambayo hayana umeme na yale yenye umeme ambayo yameshamiri kwa shughuli za biashara, hii inaonesha umuhimu wa nishati katika maeneo yote nchini." Amesisitiza Dkt.Samia

Aidha, Rais Samia ameutaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kukamilisha mapema kupeleka umeme kwenye Vijiji vilivyobaki na kuongeza kasi ya kusambaza umeme kwenye Vitongoji ili wananchi waweze kufanya kazi za maendeleo.

Aidha, amesisitiza kuwa uwepo wa umeme wa uhakika kutoka Bwawa la Julius Nyerere kunaufanya Mkoa wa Morogoro kuwa sehemu sahihi ya uwekezaji.

"Morogoro sasa ina umeme wa uhakika, hali inayovuta uwekezaji ndani ya Mkoa." Ameongeza Mhe.Rais

Akizungumzia kuhusu miradi ya umeme vijijini Mkoa wa Morogoro, Dkt. Samia amesema kupitia Wakala wa Nishati Vijijini Serikali imepeleka umeme kwenye Vijiji 621 kati ya Vijiji 669.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live