Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia atajwa maendeleo ya biashara nchini

Nauli SGR Samia atajwa maendeleo ya biashara nchini

Tue, 6 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WADAU katika sekta ya usafiri na usafirishaji wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuimarisha biashara nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dakimp International Ltd, Ally Sleyyum amesema Dar es Salaam kuwa mazingira ya biashara yanazidi kuimarika na hivyo kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi.

"Kwa muda mrefu nimekuwa katika shughuli za biashara hasa sekta ya usafirishaji, nimeona mabadiliko makubwa," alisema.

Amesema kuzinduliwa kwa Treni ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, kutasaidia ongezeko la wafanyabiashara kutoka eneo la Maziwa Makuu.

"Wateja wetu kutoka mataifa ya Maziwa Makuu sasa hawatalazimika kutumia muda mrefu barabarani, wanatumia usafiri wa SGR," alisema Sleyyum ambaye kampuni yake imekuwa ikitoa na kusafirisha mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Amesema ujenzi wa miundombinu ya barabara ya kiwango cha lami, madaraja mikoani kutasaidia kukuza uchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live