Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia aagiza bomba la gesi lipite kwa wananchi

2dd2628190c19d8f7e63c2aa189ac271 Samia aagiza bomba la gesi lipite kwa wananchi

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Nishati imesema Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza ujenzi wa mradi wa bomba la gesi kutoka Tanzania hadi Uganda upitie katika makazi ya watu ili kurahisisha ufikaji wa nishati hiyo katika maeneo ya vijijini.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Felchesmi Mramba alisema hayo juzi usiku wakati akizungumza katika kituo cha televisheni cha ITV kuhusu mafanikio ya wizara hiyo.

“Rais ameelekeza ujenzi wake upitie katika makazi ya watu ili wananchi wanufaike na gesi kama wanavyofaidika wakazi wa Dar es Salaam na sio kulipitisha katika mtaro wa bomba la mafuta kutoka Uganda,” alisema.

Alisema lengo la Rais Samia ni kuona nishati ya gesi inaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali ili Watanzania wote wanufaike na kuinua kipato chao na taifa kwa ujumla.

Mramba alisema serikali ipo katika hatua za mwisho kuanza kusafirisha gesi mikoani ikianza na Mkoa wa Dodoma ambako itajengwa bohari kubwa ya gesi itakayojazwa kwa kutumia malori.

Aidha, alisema Rais Samia ameidhinisha Sh bilioni 500 kwa ajili ya kuboresha mifumo ya umeme ili kukatika ovyo na kurekebisha maeneo ambayo mfumo umeelemewa kwa kuanzisha mfumo mwingine.

Mramba alisema katika bajeti ya 2022/23 maeneo yote nchini pamoja na visiwa vidogo vyote yatafikiwa na huduma ya umeme.

Alisema maelekezo ya serikali kwa Wakala wa Kusambaza Umeme Mijini na Vijijini (Rea) ni kuhakikisha maeneo ya huduma za jamii kama hospitali, vituo vya polisi na shule yanapata huduma hiyo kwanza.

Alisema pia serikali inafanya juhudi kubwa kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Nyerere (JNHPP) litakalozalisha megawati 2,115 za umeme ili Watanzania waanze kunufaika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live