Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia: Uchimbaji wa gesi unahitaji uwekezaji mkubwa

Gesiii Samia: Uchimbaji wa gesi unahitaji uwekezaji mkubwa

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RAIS Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa unahitajika kwenye miradi ya uchimbaji wa gesi kutokana na gharama kubwa kuanzia utafiti, uchorongaji na uendeshaji wa visima ambapo kisima kimoja ni sawa na Dola za Marekani milioni 40. - Alisema hayo jana baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame kusainiana mikataba miwili na Meneja wa Kampuni ya Maurel and Promo (E&P) Tanzania, Nicolas Engel. Mikataba hiyo ni wa mkataba wa mauziano ya hisa za kampuni ya Wentworth na mkataba wa uendeshaji wa kitalu cha Mnazibay. - Akitoa mfano Rais Samia alisema kati ya visima 96 vilivyochorongwa ni visima 43 pekee ambavyo vimepata gesi katika maeneo hayo na kuwa uendeshaji wa kisima kimoja ni sawa na Dola za Marekani milioni 550 ambayo ni sawa na bajeti ya mwaka mmoja wa wizara mbili. - Alisema kutokana na gharama kubwa za utafiti, uchimbaji na uchorongaji pamoja na uendeshaji, uwekezaji unahitajika kwani unahitajika mtaji mkubwa, ujuzi, ubobezi pamoja na teknolojia ya kisasa. Rais Samia aliipongeza TPDC kwa kununua hisa za WithWorth, lakini akaagiza kununua hisa kila wanapoona kampuni inafanya vizuri ila katika kufanya hivyo watangulize maslahi ya taifa badala ya yale binafsi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live