Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia: Siridhishwi kabisa na utendaji wa bandari zetu

Bandari Dar Es Salaam Siridhishwi kabisa na utendaji wa bandari zetu

Mon, 4 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kusuasua kwa utendakaji kazi katika bandari ya Dar es Salaam ambayo ndiyo kitovu cha biashara nchini kumemuibua Rais Samia ambaye amesema kuwa haridhishwi na uendeshaji pamoja na kazi zinazofanywa hapo.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa kipande cha nne cha reli ya SGR kinachoanzia Tabora hadi Isaka chenye umbali wa KM 165 leo Julai 04, 2022 amesema kuwa bandari hiyo ikifanya vizuri nusu ya Bajeti Kuu itatoka hapo.

"Wale tuliowakabidhi uendeshaji wa Bandari wafanye kazi kwa kasi mno, kwani siridhishwi kabisa na kazi za Bandari, Siasa na longolongo zilizopo" Rais Samia

Kauli hii imekuja kufuatia hoja iliyowasilishwa na Mkuu wa Mikoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla aliyemshukuru kwa kutoa jumla ya Tsh. bilioni 210 za maboresho ya bandari ambazo alisema kuwa zimeleta manufaa makubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live