Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia: Matumizi ya nishati safi ni lazima

Gesi Urahis Serikali Samia: Matumizi ya nishati safi ni lazima

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ili kukabiliana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia, ni lazima jamii ibadilike kifikra na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia kama gesi.

Amesema matumizi ya gesi ni lazima wala sio anasa kama ambavyo wengi wanafikiri.

Rais Samia amesema hayo leo Mei 8, 2024 mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024 - 2034.

Ametoa rai kwa wananchi kuendelea kupanda miti ili kuendeleza utunzaji wa mazingira na kufidia uharibifu wa misitu ambao umekwishatokea.

Rais Samia amewataka wananchi wasihofu kuhusu kutumia nishati ya gesi katika usongaji wa ugali, kupika maharage wala ladha ya chakula na upatikanaji wa matandu, kwani Serikali inatafuta mkakati mzuri wa kutatua yote hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live