Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salun inayotembea yazinduliwa Dar es salaam

155bef2b718ada438ecb3a96dd05ad6c Dar ya kwanza saluni inayotembea

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dar es Salaam imetajwa kuwa mkoa wa kwanza Tanzania kuanzisha huduma ya Saluni inayotembea lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Mtaalam Mwelekezi, Haris Kapiga, ameyasema hayo jana Agosti 4, 2021 wakati akizindua gari maalum ambalo ndio saluni inayotembea.

“Kwa kuwa Dar es Salaam ni Mkoa wa kwanza Tanzania katika kuanzisha huduma hii ni vyema mkatoa huduma bora zenye viwango ili mikoa mingine ivutiwe na kuja kujifunza kutoka kwenu,” alisema Kapiga na kuongeza

“Kila mtu anafanya biashara lakini kila mtu anafahamu namna ya kuwafikia wateja wake, J & R watafikia wateja makazini, watawasuka, kunyoa ndevu na huduma nyingine zote zitolewazo na saluni, wamekuja kutofautisha tupo kwenye soko la ushindani, wanakufuata ulipo,” alisema Kapiga

Aidha; Kapiga aliwataka aliwataka watumishi wa hao kufanya kazi kwa ushirikiano ‘team work’ kwa kuwa ndio nguzo kuu ya mafanikio.

“Nawaomba kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta matokeo chanya ya huduma hii,” alisema

Chanzo: www.habarileo.co.tz