Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata leseni za madini lapsua ngoma upya

Madini Pic Data Sakata leseni za madini lapsua ngoma upya

Wed, 13 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Madalali wa Madini nchini (Chammata), kimeiomba serikali kuweka utaratibu wa upatikanaji wa leseni kikanda, ili kuwarahisishia shughuli za uchimbaji kwa wafanyabiashara wadogo.

Mwenyekiti wa Chammata, Jeremia Kituyo, ametoa ombi hilo leo Julai 13, 2022 wakati wa uzinduzi wa chama hicho jijini hapa.

"Kwa sasa leseni zinakatwa kimkoa, ikimaanisha kwamba mchimbaji awe na idadi ya leseni kutokana na idadi ya mikoa anayohitaji kuchimba madini.

“Kama ni mikoa 25 ya uchimbaji, kwa mfano, ni lazima awe na idadi hiyo ya leseni na muombaji atalazimika pia kutembelea ofisi 25 za mamlaka ya mapato,” amesema.

Amesema hatua hiyo ni kwamba mbali na kupoteza muda, gharama zinakua kubwa kwani kila leseni inalipiwa Sh 250,000.

Amesema chama kimejizatiti kuwa na mchango mkubwa katika kuchangia ukuaji wa pato la taifa kupitia sekta ya madini, ikiwemo kudhibiti utoroshwaji wa madini.

"Na ndilo lengo kuu la kuanzishwa kwa chama hiki, pamoja na kuwaunganisha madalali ili kuzuia uuzaji holela wa madini," amesema.

Akizindua chama hicho kwa niaba ya Waziri wa Madini, Mkuu wa Mkoa Robert Gabriel, amesema kutokana na serikali kuwa sikivu, vipengele kwenye mwongozo wa biashara ya madini vinaendelea kutafutiwa ufumbuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live