Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la maduka ya fedha za kigeni laibuka tena bungeni

Maduka Fedha Bungeniii Sakata la maduka ya fedha za kigeni laibuka tena bungeni

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso ameitaka Serikali kueleza hatma ya fedha na vifaa walivyovichukua katika maduka ya kubadilishia fedha za kigeni.  

Pareso amehoji hayo leo Juni7, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2022/2023.

Amesema mwaka 2018, Serikali ilichukua fedha na vifaa vya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ikiwamo komyuta, mashine za EFD na baadhi ya wafanyabiashara walichukuliwa hati.

Amesema hiyo ni mara ya nne kutaka kupata kauli Serikali kuhusiana na wafanyabiashara hao ambao wameporwa fedha zao tangu mwaka 2018.

Hata hivyo, amesema hakuna muafaka wowote uliofikiwa kuhusiana na jambo hilo na kuitaka Serikali kueleza ni lini Serikali itafikia muafaka kuhusiana na mashauri ya wafanyabiashara hawo.

“Mmeunda taksi force mkaenda tena kwa wafanyabiashara kuwaambia kuwa mnadaiwa sasa mmechukua kila kitu halafu mnaenda kuwadai tena.

Mnafanya kazi kwa taksiforce ya kutishia watu na si kuleta muafaka ili watu wafanye biashara kwa amani na utulivu,”amesema.

Ameomba kupatiwa majibu ya Serikali ya kina na kweli kuhusu jambo hilo kwa kuwa wafanyabiashara hao wanataka kufahamu hatma mlizozichukua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live