Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sajilini biashara muwe Kwenye mfumo rasmi

A46a0e538c8c0010ca2875a55d30d51d Sajilini biashara muwe Kwenye mfumo rasmi

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Taasisi za Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Anjelina Ngalula amewataka wafanyabiashara kusajili biashara zao ili waingie katika mfumo rasmi unaotambulika kisheria.

Ngalula alisema hayo kwenye Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonyesho ya Bidhaa yanayoendelea Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambayo yanamalizika Jumapili.

Alisema Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), ipo kwa ajili ya kuwahudumia wafanya biashara ni taasisi ya serikali ambayo imeboresha huduma zake kwa kuwa mtu anaweza kujisajili kupitia mtandao tofauti na ilivyokuwa zamani na kupata cheti chake kwa haraka.

“Tunawaomba wafanyabiashara wale wanaotaka kusajili biashara zao wahakikishe wanakuwa na zile nyaraka muhimu zinazotakiwa ili iwe rahis kwao kujisajili.

“ Nasema hivyo kwa sababu kumekuwa na Malalamiko kwa watu kuwa kuna changamot katika kujisajili lakini kumbe inatokana na nyaraka zinazohitajika kutojitosheleza,” alisema.

Aliwapongeza Brela kwa kuwepo katika shughuli yao hiyo ya sekta binafsi ya wanawake kwa sababu inaonyesha ni jinsi gani ilivyo karibu na wafanyabiashara.

“Tayari wakina mama wameiitika na kusajili biashara zao ndio kitu tunachokipigania kila mara watu watoke kwenye mfumo usio rasmi waje kwenye mfumo rasmi, watoke huko ambako hawatambuliki ambapo huwezi kupata mkopo kama hujajisajili na biashara yako haijulikani,” alisema.

Alisema kujitokeza kwa wingi kwa wafanyabiashara kwenye maonyesho hayo kujisajili na wakala huo ni hatua kubwa katika biashara zao.

Kwa upande wake Ofisa leseni wa Brela, Sweetnes Madata alisema huduma wanazozitoa ni pamoja na kusajili biashara, makampuni , alama za biashara pia wanatoa leseni za biashara na leseni za viwanda.

Alisema ili mfanyabiashara asajiliwe anapaswa kuwa na nyaraka muhimu ikiwemo namba ya kitambulisha cha Taifa (NIDA), uthibitisho wa eneo analokaa, pamoja na taarifa za biashara yake.

Alisema wapo kwenye maonyesho hayo kuwa karibu na wajasiriamali ili wawasaidie kurasimisha biashara zao zitambulike kisheria pamoja na kuwapa ushauri mbalimbali wa jinsi ya kurasimisha biashara zikiwa zimetambulika na faida zake

Alisema toka maonyesho hayo yalipoanza wamesharasimisha biashara nyingi na wataendelea mpaka siku ya mwisho ya Jumapili.

“Tumewazungukia wafanyabiashara mbalimbali na kuwaelimisha huduma zetu wamekuja kusajili,” alisema.

Mfanyabiashara Marcelina Biro alisema amefika katika viwanja hivyo na kufanikiwa kusajili biashara yake kwa muda mfupi kisha kuondoka na cheti.

Chanzo: www.habarileo.co.tz