Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Safari ya uchumi wa viwanda kwa wanasayansi haihitaji mzaha’

9529 Safari+pic+2 TZWeb

Tue, 19 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imesema kama Taifa linataka kufanikiwa katika safari ya uchumi wa viwanda, suala la kuwainua wataalamu wa sayansi si la kufanyia mzaha.

Akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha nne, mwaka 2016 na cha sita wa mwaka 2017, waliofanya vizuri masomo ya baiolojia na kemia, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Kambi alisema taaluma hizo ni msingi wa Tanzania ya viwanda.

Kambi alikuwa akimwakilisha Naibu Waziri wa Afya, Faustine Ndugulile.

“Taaluma hizi zinajulikana kama msingi wa sayansi na teknolojia ambayo inazalisha wataalamu wanaotumika viwandani, watafanya kazi za uchunguzi wa kimaabara au kutoa huduma za tiba, hospitalini,” alisema.

Alifafanua kuwa maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilianzisha utaratibu wa kuwatunuku wanafunzi bora pamoja na walimu wao waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya kidato cha sita na nne pamoja na walimu wao zaidi ya miaka 10 iliyopita.

“Utaratibu huo tangu ulipoanzishwa, umeongeza ushindani kati ya shule na shule, walimu na walimu na wanafunzi kwa wanafunzi hali inayoongeza idadi na ufaulu wa wanafunzi katika masomo hayo,” alisema Profesa Kambi.

Alifafanua kuwa uwapo wa wataalamu wa kutosha katika taaluma hizo ndiyo msingi pekee wa maendeleo katika Taifa lolote.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk Fidelice Mafumiko alisema kwamba kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi katika katika mitihani yao ya Taifa kwa masomo ya kemia na baiolojia kunaleta chachu ya kupenda zaidi masomo ya sayansi.

Alisema kwamba tangu kuanza kwa utaratibu huo mwaka 2007 hadi sasa, mamlaka imetoa zawadi kwa jumla ya wanafuzi 168 pamoja na walimu 12.

Chanzo: mwananchi.co.tz