Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sado zaleta kasheshe wakulima, wafanyabiasha Siha

Sado Kasheshe Sado zaleta kasheshe wakulima, wafanyabiasha Siha

Sun, 17 Sep 2023 Chanzo: Mwananchi

Wananchi wa Kijiji cha Donyomurwa kata ya Donyomurwa Wilaya Siha mkoani Kilimanjaro, wametaka kuchukuliwa hatua kwa wafanyabiashara wilayani humo wanaoendelea kununu mazao ikiwamo mahindi na maharage kwa kutumia sado badala ya mizani kama Serikali ilivyoagiza lengo la kumuepusha mkulima kupata hasara.

Malalamiko hayo yametolewa leo Jumapili septema 17, 2023 na wananchi hao wakati wa ziara ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi ikiwa ni muendelezo wa kutembea miradi na kusikiliza kero za wananchi kwenye vijiji vyote wilayani humo.

Wananchi hao wakizungumza mara baada ya kupewa fursa ya kusema kero zao, wamataka serikali kuwachukulia hatua watu hao badala ya kuwaangalia wakiendelea kuwaumiza wakulima ili waachane na tabia hiyo.

"Tunaomba mizani itumike tunaumia sana, tunatumia gharama kubwa hadi kuvuna lakini wafanyabiashara wakati wa kuwauzia.

“Kibaya zaidi wafanyabiashara mwaka huu wamekuja na kipimo wanakiita kitoto ndoo, unakuta sisi tunateseka kulima tunatumia gharama chochote kile tunachoapata kidogo ukitaka kuuza kikusaidie kimechukuliwa na wafanyabiashara,” amesma mkulima Joseph Leitayo.

Catherine Mollel, ameomba Serikali pamoja na kitengo cha kilimo kupita masokoni na vijiji kwa wakulima kutoa elimu ya namna ya kutumia mizani na faida yake iili tatizo liweze kuondoka.

Mollel amesema ukiuza gunia moja la mahindi kwa kutumia vipimo vyao kiuhasilia umeuza gunia moja na debe moja na nusu au zaidi, “Tunaomba serikali ilisimamie jambo ili kumnusuru mkulima apate faida ya kile alichokifanyia kazi na kuendelea kuwa na moyo wa kilimo,”

Katibu wa CCM Wilayani humo, Ally Kidunda amesema Baraza la madiwani halmshauri lilishazuia biashara hiyo na maelekezo yalitoka kutumia mizani.

"Baraza walishazuia biasha hiyo na kutoa maelekezo kutumia mizani, taongea na mkurungenzi mtendaji wa halmshauri atoe maelekezo kwa watendaji wa kijiji kusimamia zoezi hilo," amesema Kidunda.

Joyce Mmar mfanyabiashara wa mazao amesema baadhi yao wameshaanza kutumia mizani lakini amedai tabia hujenga mazea, “Tumezoea kutumia sado, sasa hii ya mizani tunaona kama faida ni ndogo tutazoea,”

Naye Ofisa Kilimo wilayani Siha, Habibu Ally amewataka wakulima kutoa taarifa wanapoona mfanyabiashara amefika katika maeneo yao kununua mazao kwa kutumia sado.

Amesema mpaka sasa sado kadhaa wamezichukua kutoka kwa wafanyabiashara “Tunaomba ushirikiano kwa wakulima na tunaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wakulima hao ili kufikia lengo,”

Chanzo: Mwananchi