Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za Watanzania kuwa wachache wanaoongoza kampuni zatafutiwa ufumbuzi

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ushiriki wa Watanzania katika kuongoza kampuni za kimataifa zilizowekeza nchini humo umetajwa kuwa mdogo kwa kuwa nafsi ya maofisa watendaji wakuu zinashikiliwa na wageni.

Hayo yalibainishwa leo Jumatatu Agosti 26, 2019 na Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni Binafsi nchini (CEOrt) wakati wa hafla ufunguzi wa mafunzo ya kuwaandaa maofisa watendaji wakuu wa baadaye.

Mkurugenzi Mtendaji wa CEOrt, Santina Benson amesema kati ya kampuni wanachama 150 wa umoja huo asilimia 47 ya kampuni hizo zinaongozwa na raia kutoka nje ya nchi na ushiriki wa wanawake ni mdogo zaidi.

“Maofisa watendaji wakuu wengi ambao ni Watanzania wapo katika kampuni za Kitanzania na wengine wameanzisha hizo kampuni wenyewe, tunaona haja ya kuongeza wigo kwa Watanzania kushikilia nafasi hizo,” amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Trademark Afrika Mashariki, John Ulanga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya mafunzo ya kuwaandaa maofisa watendaji wakuu amesema katika nchi nyingine viongozi hao hutengenezwa.

“Katika nchi nyingine ni kawaida kuwatengeneza viongozi, inapotokea nafasi hiyo katika kampuni fulani watu wanakuwepo tayari, watu hao wanakuwa na ujuzi, vigezo na haiba ya kuongoza kwani kigezo sio elimu pekee,” amesema Ulanga.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz