Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za Tanzania kuilipa kampuni ya Canada fidia ya bilioni 76

Pesa Fedhaddd Sababu za Tanzania kuilipa kampuni ya Canada fidia ya bilioni 76

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania imelipa dola milioni 30 (TZS bilioni 76.5) kwa Kampuni ya Canada ya Winshear Gold Corp ili kumaliza mgogoro wa uwekezaji na kampuni hiyo nje ya mahakama.

Winshear iliyokuwa ikiendesha mradi wa dhahabu Kusini Magharibi mwa Tanzania ilifungua kesi katika Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID), ikitaka karibu dola milioni 100 [TZS bilioni 250.5] kama fidia kutoka kwa serikali ya Tanzania baada ya kufutwa kwa leseni yake ya kuhifadhi madini.

Kwa kutatua mgogoro huo nje ya mahakama, Serikali ya Tanzania imelenga kupunguza kuharibika kwa sifa ya nchi kama eneo la uwekezaji na kuepuka kutumia muda mwingi na pesa nyingi ambazo zingetumiwa ikiwa kesi ingeendelea hadi mwisho.

Kwa upande mwingine, Winshear imesema katika taarifa yake kwamba baada ya kukatwa gharama zake za kisheria, imepata kiasi cha dola milioni 18.5 [bilioni 46] kutoka kwenye dola milioni 30 zilizolipwa na Tanzania.

Katika Serikali ya Awamu ya Tano ya Hayati Rais John Magufuli ilitangaza mageuzi ya sheria za madini na kupitisha sheria ya marekebisho ambayo miongoni mwa mambo mengine ilifuta leseni za uhifadhi madini.

Kufuta leseni za madini kulikiuka Mikataba ya Uwekezaji baina ya Nchi Mbili (BITs) ambayo Tanzania ilisaini na nchi kadhaa za kigeni, inayolinda wawekezaji kutoka nchi hizo kwa kuzuia hasara ya haki zao na mali, pamoja na leseni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live