Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya ya bei ya nondo na misumari kupaa

Nondo Vifaa Ujenszi Sababu ya ya bei ya nondo na misumari kupaa

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nabi Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amesema kupanda kwa bei ya nondo na misumari kumetokana na uhaba wa chuma ghafi na chakavu ambavyo ndio malighafi inayotumika kutengenezea bidhaa hizo.

Kigahe alibainisha hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi aliyehoji sababu za kupanda kwa bei ya bidhaa hizo.

Naibu Waziri huyo alisema kupanda kwa bei kunategemeana na soko la chuma duniani, akiwa na ufafanuzi kwamba  viwanda vingi kwa sasa vinategemea chuma ghafi toka nje ya nchi.

"Bei hizi ni za kimataifa, ndio maana unaona bei inaongezeka, ndio maana tumeruhusu hata chuma chakavu kutoka nje kuuzwa hapa (nchini) ili kusaidia (kukabili) huo upungufu.

"Tunajitahidi kutoa taarifa sahihi kwa wakati kwamba kuna changamoto hizo na mpango wa serikali ni upi katika kuhakikisha bei inashuka.

"Tunachokifanya sasa ni kupata wawekezaji kuzalisha chuma ghafi, kwa sababu chuma kinapotoka nje ya nchi, kinakuja kwa gharama zinazosababisha ongezeko kwa mlaji wa mwisho," alifafanua.

Naibu Waziri Kigahe alitaja jambo lingine linalochangia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kuwa ni mahitaji ya soko kwa walaji; wauzaji wengi wanaangalia namna walivyoipata bidhaa hiyo na wauzaje ili wapate faida.

Kiongozi huyo pia aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kununua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

"Wenye viwanda pia wanatakiwa kuzalisha bidhaa bora na zenye bei rafiki, kama hazitakuwa na ubora tutashindwa kushindana na zile za kutoka nchi jirani.

"Hatari ninayoiona kama wakiendelea kuzalisha bidhaa zisizo na ubora, wateja watakimbilia zile za kutoka nje ya nchi, hali itakuwa mbaya sana kwa ustawi wa nchi na viwanda," alihadharisha.

Kumekuwa na malalamiko toka kwa wananchi kwamba bei ya nondo na misumari imepanda katika maeneo yao, baadhi wakidai kuna ongezeko la Sh. 2,000 katika kila nondo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live