Taasisi ya Uongozi na Maendeleo ya Ujasiriamali (Imed) imesema, miradi mingi ya biashara inakufa katika hatua za awali kutokanana na kukosa mafunzo atamizi ya ujuzi wa biashara.
Kutokana na hali hiyo taasisi hiyo imeendesha mafunzo atamizi ya siku nne kuanzia Mei 16 hadi 19 kwa lengo la kuwajengea uwezo wanasanifu, mameneja, watumishi, wataalamu wa fedha, makandarasi na wakufunzi katika kusanifu, uongozi na kuendesha miradi kwa mafanikio.
Mkurugezi wa Imed, Dk Donath Olomi, amesema lengo la mafunzo hayo ni kukabilina na changamoto ya ajira kwa kuwapa mafunzo ya jinsi ya kuendesha miradi ya biashara katika katika hatua za awali.
“Tumetoa mafunzo kwa watu 22 kutoka kwenye taasisi zenye atamizi kama za biashara ya usaifu, ikiwa pamoja na kufanya upembuzi yakinifu, kutayarisha mipango mikakati ya biashara na kuatamia watumishi,” amesema.
Amesema atamizi za biashara ni pamoja na huduma zilizoandaliwa kukuza biashara zinapokuwa katika hali ngumu.
“Ni mkakati endelevu wa kusaidia uanzishwaji na ukuaji wa biashara ili kukabliana na changamoto ya ajira,” amesema.
Amesema mafunzo hayo ya siku nne yalihusisha washirki kutoka Tanzania, Sweden na Uganda kutoka taasisi za Serikali, kampuni binafsi, Mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za fedha zikiwemo Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM), Kituo cha ubunifu wa Kilimo (AIC) chiniya PASS, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Rikolto, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (Taliri) na Soft Net.
Wataalamu wa kutoka Tanzania Renewable Energy Business Incubator (Tatebi, Sahara Ventures na Uganda Renewable Energy Business Incubator (Rebi) wametoa mafunzo katika warsha hiyo.