Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu wakulima wa korosho kuchelewa kulipwa na Serikali ya Tanzania zatajwa

74860 Korosho+pic

Mon, 9 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema itamaliza deni la wakulima wa korosho kabla ya msimu ujao kuanza.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Septemba 9, 2019 bungeni mjini Dodoma na naibu waziri wa Kilimo,  Omary Mgumba wakati akijibu swali la mbunge wa Ndanda (Chadema) Cecil Mwambe.

Mwambe amehoji ni lini watakamilisha madeni ya wakulima wa korosho kwa kuzingatia Serikali ilisema inazo fedha za kuwalipa.

Katika majibu yake Mgumba amesema kilichotokea ni Bodi ya Mazao Mchanganyiko kuwa imefikia kikomo cha kuchukua fedha katika Benki ya Uwezeshaji nchini (TIB).

Amesema TIB waliwataka kuuza kwanza korosho walizonazo ambazo tayari zimeshauzwa na kwamba kabla ya msimu wa korosho kuanza wakulima hao watakuwa wameshalipwa fedha zao.

Katika swali la msingi mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amesema ni kweli bei ya bidhaa za viwandani kwa kiwango kikubwa zinatokana na gharama za uzalishaji kama  maji, umeme na nguvukazi.

Pia Soma

Advertisement

“Je kitendo cha kutoa kibali kwa viwanda vya sukari kuagiza sukari kutoka nje sio kuua kabisa kilimo cha zao la miwa ambacho wakulima wanategemea kuuza kwenye viwanda vya ndani,” amehoji Kubenea.

Akijibu swali hilo Mgumba amesema  mfumo wa kuwapa leseni wazalishaji wa ndani kuagiza sukari kutokana na mahitaji umeweza kudhibiti uingizaji wa sukari ya ziada nchini kwani wazalishaji huagiza kulingana na kiasi kilichoainishwa kwenye leseni husika.

“Kabla ya utaratibu wa kuwapa vibali wenye viwanda kuagiza sukari nakisi ya sukari ilikuwa ni zaidi ya tani 130,000 lakini baada ya utaratibu wa wenye viwanda kuagiza upungufu umepungua hadi kufikia tani 38,000,”amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz