Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu mradi wa gesi kusimama zatajwa

77368 Gesi+pic

Fri, 27 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Naibu Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Subira Mgalu amesema mradi wa ujenzi wa kiwanda cha uchakataji na uuzaji wa gesi iliyo katika kimiminika mkoani Lindi ulisimama kutokana na kampuni kutoelewana katika mazungumzo.

Mgalu ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 26, 2019

mkoani Mtwara katika mkutano kati ya mawaziri, taasisi za umma na binafsi, wafanyabiashara na wadau wengine kusikiliza changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi.

Waziri Mgalu amesema Serikali kama wabia na mradi huo mkubwa wa zaidi ya dola bilioni 30 za Marekani walikubaliana na hao wabia na kuanza mazungumzo.

“Uzoefu unaonyesha mazungumzo ya mradi mkubwa kama huu unachukua mpaka miaka saba hivi lakini sisi matarajio yetu mwaka 2022 mradi utaanza na kukamilika mwaka 2028, kwa hiyo mtaona huu mradi ni mkubwa lazima mazungumzo yaendelee,” alisema Mgalu

Amesema gesi ni uwekezaji wa viwanda na mbolea na kwa kuwa Mkoa wa Mtwara ni mdau halmashauri zote ziliingia mkataba na kupewa asilimia tano.

Pia Soma

Advertisement
Awali,  mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mtwara, Said  Swallah amesema kusimama kwa utekelezaji wa mradi huo  kumepoteza matumaini ya wafanyabiashara wengi walioitikia wito wa Serikali kuchangamkia fursa ya uwepo wa miradi mikubwa ambayo iliibuka na kutekelezwa kati ya mwaka 2010 hadi 2014.

“Hali imebadilika ghafla hata ukifanya ufuatiliaji wa karibu kwa kuangalia viashiria vya kuathirika kwa biashara katika Mkoa unaweza kubaini ni kwa kiasi gani baada ya kusimamia kwa shughuli za uwekezaji katika sekta ya gesi na mafuta zinaonekana bayana, moja kati ya maeneo hayo ni sekta hiyo ni hoteli na nyumba za kulala wageni,” amesema Swallah

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz