Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SUA kuja na mbinu mpya kilimo cha kisasa

Maharage Kilimo.jpeg SUA kuja na mbinu mpya kilimo cha kisasa

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeendelea kuzalisha vijana wanaojiajiri katika shughuli za kilimo ili kuwa na uhakika wa chakula nchini na kuuza nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa SUA, Profesa Raphael Chibunda wakati wa kipindi cha Jambo Tanzania cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akizungumza juu ya Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru linalofanyika chuoni hapo.

Chibunda amesema SUA imeendelea kuzalisha wataalamu na watafiti wenye uwezo mkubwa katika sekta ya kilimo na kuleta mageuzi ya kilimo nchini kwa kushirikiana na Watanzania na wataalamu wengine nje ya nchi.

Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeongeza nguvu kubwa kukisaidia chuo hicho kufundisha na kufanya tafiti nyingi zinazosaidia Taifa katika sekta ya kilimo na ufugaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live