Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

STAMICO yapunguza utegemezi kwa 87%

6bdc49e67c2fb695c38af1d0980502c5 Waziri wa Madini, Doto Biteko

Fri, 11 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) limepunguza utegemezi kutoka Serikali Kuu kutoka utegemezi wa asilimia 100 Hadi asilimia 13 Waziri wa Madini, Dk Doto Biteko alisema hayo jana Dodoma wakati akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema kwa sasa STAMICO imekuwa ikitekeleza miradi, inafanya biashara na kusisitiza kuwa hivi karibuni imesaini mkataba wa uchorongaji kati yake na Buhemba Gold Company wenye thamani ya Sh bilioni 11.5.

“Kandarasi hii inahusu kuchoronga mita 10,000 za miamba kwa teknolojia ya DD na mita 30,000 kwa teknolojia ya RC.” alisema Dk Biteko.

Alisema mkataba mwingine ni wa makubaliano ya utafiti na uendelezaji wa leseni za madini za Shirika na kampuni ya ASME ya Singapore wenye thamani ya karibu dola za Marekeni milioni 300.

“Tayari shirika limefanya uchorongaji katika mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) wenye thamani ya shilingi bilioni 18 na katika Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) shilingi bilioni 1.4.”

Dk Biteko alisema STAMICO pia imeanzishwa uzalishaji mkubwa wa dhahabu katika Mgodi wa dhahabu wa Buckreef uliopo Geita, kuendeleza mradi wa kuchimba Dhahabu Buhemba kwa kutengeneza miundombinu ya mgodi, kuagiza mtambo na shughuli za uchorongaji.

Pia, Shirika limeweza kutoa gawio serikalini la jumla ya Sh bilioni 1.2 katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Dk Biteko alisema shirika hilo limekusanya Sh bilioni 19.97 kati ya Machi 2021 na Februari 2022 kutoka vyanzo vyake vya ndani.

Kwa upande wa Tume ya Madini, Dk Biteko alisema serikali imetoa Sh bilioni 11.28 ili kununua magari na vifaa vya masoko kwa lengo la kuongeza wigo wa kukusanya maduhuli ya serikali na kuboresha utekelezaji wa majukumu ya tume.

Dk Biteko alisema Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), imeimarisha kwa vifaa hivyo kuongeza kasi ya uchunguzi wa sampuli na tafiti za madini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live