Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SMZ yatangaza bei ya karafuu

A784a7899941c225e465f7e761d0b956.png SMZ yatangaza bei ya karafuu

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza bei ya kununulia karafuu kutoka kwa wakulima kwa ajili ya msimu wa mavuno unaotarajiwa kuanza mwezi ujao na kilo moja itanunuliwa kwa Sh 14,000.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban, ametangaza bei hiyo na kusema mkulima atakayeuza karafuu atafaidika na asilimia 80 inayopatikana katika soko la dunia.

Aidha alisema karafuu ya daraja la pili itanunuliwa kwa Sh 13,000 wakati daraja la tatu ni Sh 12,000.

Alisema katika msimu wa mavuno wa mwaka huu watanunua karafuu kutoka kwa wakulima na kuwaingizia fedha zao kupitia akaunti za benki au kwa njia ya malipo ya simu.

Alisema wameamua kuchukua uamuzi huo kwa ajili ya kuepusha matukio ya uhalifu na utapeli wanaoweza kufanyiwa wakulima.

Alisema vituo vya kununulia karafuu vipo katika mikoa yote miwili ya Pemba katika miji mitatu na kwa upande wa Unguja zitanunuliwa katika kituo cha Saateni.

Chanzo: www.habarileo.co.tz