Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SMZ yakoshwa utendaji ATCL

ATCLL SMZ yakoshwa utendaji ATCL

Fri, 10 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema imeridhishwa na utendaji wa uongozi wa Kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ambapo mageuzi makubwa yaliyofanywa yameiwezesha kampuni hiyo kuingia katika ushindani wa kibiashara wa kimataifa.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Khalid Salum Mohamed amesema wakati akifungua mkutano wa pili wa baraza la wafanyakazi kampuni ya ATCL Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana. Alisema ATCL imeingia katika mageuzi makubwa mwaka 2016 kutoka ndege moja hadi kufikia ndege 12 zilizopo sasa zikiwemo Airbus mbili.

Aidha, alisema kutoka vituo vinne vya kutoa huduma katika mikoa ya Jamhuri ya Muungano hadi kufikia vituo 14 ikiwemo 10 vilivyopo nje ya nchi. Alisema mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na uwajibikaji na utendaji pamoja na ubunifu katika sekta ya biashara katika masuala ya ndege.

‘’Tumejipanga kuifungua Pemba kiuchumi na uwekezaji ambapo sehemu ya mikakati hiyo ni ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Pemba ili kukidhi viwango vya kimataifa,’’ alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live