Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SMZ yajifunza kuongeza upatikanaji wa maji Bara

Smzpic Data SMZ yajifunza kuongeza upatikanaji wa maji Bara

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Katika kufikia lengo la kuongeza upatikanaji wa maji kufikia asilimia 75 katika mwaka huu wa fedha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo kujifunza kinachofanyika Tanzania Bara.

Kwa sasa upatikanaji wa maji visiwani humo ni asilimia 55 lakini tayari wameshaanza kutekeleza miradi ambayo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu itaongeza asilimia 20.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini,  Dk Mngereza Mzee Miraji wakati watendaji wa wizara hiyo, Mamlaka ya Maji Zanzibar (Zawa) na wajumbe wa baraza la wawakilishi walipotembekea mradi wa visima vya Kimbiji unaotekelezwa na  Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa).

Dk Miraji ameeleza  kuwa pamoja na kuwa na uhakika wa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji upo umuhimu wa kujifunza namna ya kukabiliana na upotevu na kuhakikisha maji hayo yanawafikia wananchi.

Amesema  lengo la SMZ ni kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi na salama hivyo haitachoka kutafuta namna bora ya kufanikisha lengo hilo.

“Tumekuja huku kujifunza, maji sio wizara ya muungano lakini kwa kuwa wenzetu bara wamepiga hatua tumeona tuingie makubaliano ya kushirikiana na kushirikishana uzoefu.

Advertisement “Kuna maeneo mengi ambayo wenzetu bara wamepiga hatua ikiwemo uendeshaji wa hizi mamlaka za maji ndiyo maana tukaona tuje kujifunza Dawasa ili hata hicho kiwango kikiongezeka basi kiwafikie wananchi na kupunguza changamoto za hapa na pale,” alisema Dk Miraji.

Naye makamu mwenyekiti wa kamati ya mawasiliano, ardhi na nishati Huzaima Mbaraka alisema katika ziara hiyo wamebaini kuwa mafanikio yaliyopo kwenye sekta ya maji Tanzania bara ni kutokana na watendaji kujitoa kikamilifu.

“Tumeona kwamba watendaji na wafanyakazi kwenye sekta wameamua kujitoa kwa dhati kufanya kazi na kuwa wabunifu katika kuhakikisha sekta inasonga mbele.

“Tunamaamini ari hii ikiwepo Zanzibar tutafika mbali lakini kwa kuwa sisi ni wawakilishi tunachukua hili na kwenda kywashauri wenzetu waone umuhimu wa kufuata mfano huu lengo likiwa moja kutoa huduma stahiki kwa wananchi,” amesema Huzaima.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja amesema mamlaka hiyo iko tayari kushirikiana na mamlaka za maji za Zanzibar na kushirikishana uzoefu

Akizungumzia mradi wa maji wa visima vya Kimbiji amesema  utazinduliwa wakati wa wiki ya maji na wakazi wa Kigamboni wataanza kupata maji hayo kuanzia Aprili mwaka huu.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz