Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SIDO yaingilia kati mikopo kausha damu

Pesa Fedhaddd SIDO yaingilia kati mikopo kausha damu

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini (SIDO) limesema linaendelea kusaidia kupunguza mikopo ya Kausha Damu kwa Kutoa Huduma za Kifedha kupitia Utoaji Elimu wa namna ya Upatikanaji wa Mitaji na Usimamizi wa Fedha, Mikopo midogo ya ndani, pamoja na Mkopo aina ya Current Guarantee Scheme (CGS).

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika La SIDO Mkoa wa Kilimanjaro Allen Yotham Mhidze wakati wakimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hilo katika Maonyesho ya kwanza kwa Wafanyabiashara Wilayani Pangani, mkoani Tanga

Amesema njia ya Kuwasaidia wananchi kuondokana na Mikopo ya Kausha Damu na kuwasadia katika Kukuza na Kuinua Uchumi wao ni pamoja na kuhahakikisha wanatoa Ushauri wa Kiteknolojia sambamba na kuwapatia vifaa vya Teknolojia mbalimbali za Uchakataji wa Mazao, pamoja na uanzishaji wa Viwanda mbalimbali utakaosaidia Wilaya hiyo kuchangia Uchumi wa Taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live