Menu ›
Biashara
Tue, 30 May 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Serikali imeratibu majadiliano kuhusu kushirikiana na Burundi katika ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza (Tanzania) hadi Gitega (Burundi).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stergomena Tax amesema hayo wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/2024 bungeni mjini Dodoma leo (Mei 30, 2023).
Mradi huo ambao unatarajiwa kutekelezwa kupitia ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) utakapokamilika utaunganisha Tanzania na nchi jirani za Burundi, Rwanda na DRC.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live